Sunday, 15 December 2019

AFYA: WALI NI HATARI ZAIDI KULIKO SODA KATIKA KUSABABISHA KISUKARI, FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA



Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kisukari mamlaka nchini Singapore zimeeleza kuwa mchele mweupe ni hatari zaidi kama kisababishi cha ugonjwa huo kuliko hata soda.
Watalaamu wa afya wameeleza kuwa kiribatumbo au vinywaji vyenye sukari ni visababishi vikubwa pia vya ugonjwa huo, hasa katika nchi za Magharibi. Lakini kwa upande wa nchi za Asia wali mweupe umekuwa ni tatizo kutokana na starch katika chakula hicho ambapo huijaza miili ya walaji na kiwango kikubwa cha sukari katika damu, na hivyo kuongeza hatari ya kupata Kisukari.
Katika tafiti nne zilizofanywa na Harvard School of Public Health na kuchapishwa katika jarida la afya la nchini Uingereza zilibaini kuwa, moja kila sahani moja ya wali inayoliwa kwa siku inaongeza uwezekano wa kupata kisukari kwa 11% kwa ujumla.
Pili, wakati raia wa Asia mfano wachina wakila wale kwa wastani wa mara nne kwa siku, wakazi wa Marekani na Australia hula chakula hicho kwa wastani wa mara tano kwa wiki.
Kutokana na hatari kubwa inayotokana na ulaji wa mchele mweupe, wataalamu wanashauri watu kupunguza kiwango cha ulaji wa chakula hicho. Mbali na hilo ambalo kwa baadhi ya watu linaweza kuwa gumu, wanashauriwa kuchanganya wali mweupe na wali wa ‘brown’ ili kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Ugonjwa wa Kisukari huchangia kupoteza uwezo wa mtu kuona, figo kushindwa kufanya kazi, pamoja na matatizo mengine ya kiafya.
Kuweza kujikinga na ugonjwa huo watu wanashauriwa kupunguza kiwango cha ulaji wa mchele mweupe, vinywaj vyenye sukari, pamoja na vyakula vya kisasa (junk foods).

Saturday, 7 September 2019

MFAHAMU MWANAMKE MWENYE CHEO KIKUBWA ZAIDI JWTZ



Anaitwa Major General Zawadi Madawili, ni mtoto wa mzee Madawili aliyewahi kuwa miongoni wa viongozi maarufu wa chama cha TANU mkoani Iringa.
Mama Madawili ni mzaliwa wa tarafa ya Malangali wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Major General Zawadi Madawili

Major General Zawadi Madawili ni afisa mstaafu mwanamke wa jeshi la wananchi wa Tanzania {JWTZ}. Madawili alikuwa mwanamke wa kwanza wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ} kuwa luteni toka mwaka 1975. Aliweza kuwa na cheo cha brigedia mkuu mwaka 2003.

Madawili aliweza kuripotiwa katika Mpango wa ndani ya Jamhuri ya Muungano wa kuondoa athari za kiuchumi ndani ya nchi na bara. Madawili pia aliweza kuanzisha jitihada zilizofanywa na uharakati wake kuchochea hisia za wanawake wa Tanzania kuanzisha mpango wake.
Madawili alifikia cheo cha Major General kabla ya kustaafu kwake jeshi.

Mnamo Oktoba 2017 alichaguliwa kwenye bodi ya kuwezesha Huduma za Jamii ambayo ilikuwa imeanzishwa katika kulipia watumishi wa uma

Major General Zawadi Madawili ndiye Mwanamke mwenye cheo kikubwa zaidi JWTZ.
Huyu mama amepiga kozi nyingi sana hadi kufikia hapo alipo, anastahili pongezi.

Leo, mzalendo hadi kuruti wa kike wote wanaitwa MADAWILI kwa HESHIMA yake
This is a ROLE MODEL! Who The people, our daughters should know about.



Monday, 24 June 2019

CHADEMA YAMVUA UANACHAMA DKT. MAKONGORO MAHANGA

Chama cha Demokarasia na Maendeleo (Chadema) kimemvua uanachama Dk. Makongoro Mahanga baada ya kubainika anakihujumu chama hicho pamoja na kutoa siri za chama kuzipeleka CCM.
Mwenyekiti wa Chadema tawi la Migombani jimbo la Segerea, Baraka Mwalukunga, alisema wamegundua ni msaliti ndani ya chama na kuamua kumvua uanachama.

Alisema waliweka kikao cha mwenendo wa nidhamu cha kumjadili Dk. Mahanga baada ya kuitwa katika vikao mbalimbali ili kutoa utetezi juu ya tuhuma anazomkabili ama kujieleza jinsi anavyofanya makosa ndani ya chama.

“Amekuwa akikaidi, kudharau vikao vya chama hivyo kutokana na mwenendo wake wa usaliti na kufanya mapinduzi ndani ya chama kwa mujibu wa katiba ya chama ibara ya 5 (4) kifungu cha tatu natangaza kumvua uanachama tangu Juni 21 mwaka huu,” alisema

Aliongezea kuwa:”Kwa mamlaka hiyo Dk. Mahanga sio mwanachama wa Chadema tumechoka na usaliti wake,”

Dkt. Makongoro Mahanga

Alisema Makongoro Mahanga amekuwa akikiuka katiba kanuni na kosa kubwa ni usaliti na amekuwa akitoa siri za chama na kuzipeleka CCM na ushahidi wanao kwani vikao hivyo alikuwa akivifanya nyumbani kwake.

Aidha, Mwalukungu alisema Mahanga amekuwa akisababisha migogoro kwa namna anavyotaka yeye na kuwaondoa wanachama bila kufuata utaratibu.

Alisema wamemuita ili aweze kutoa utetezi lakini amekuwa ni mkaidi na kudharau mamlaka ya chama.

Alisema Mahanga alikuwa akifanya mambo mbalimbali ya kukihujumu chama na kujikuta wakitumia nguvu kubwa ya kupambana wakati taarifa hizo anazifanya akiwa nyumbani kwake.

“Usaliti ni kosa kubwa kuliko mengine tawi limeridhia kumuondoa kitendo cha kukataa kutii ngazi ya tawi hawezi kuendelea kuwa mwanachama,” alisema.

Mkongora Mhanga alishawahi kuwa Mbunge wa Ukonga kuanzia mwaka 2000 hadi 2010 ambapo jimbo hilo liligawanyika na kuzaliwa jimbo la Segerea ambapo aliongoza katika kipindi cha miaka mitano.

Mahanga alishawahi kuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira na baada ya hapo alihama chama cha CCM na kuhamia Chadema ambapo alikuwa ni Mwenyekiti wa chama (Chadema) mkoa wa Ilala.
               

Friday, 21 June 2019

TAARIFA YA JESHI LA POLISI TZ KUHUSU LOSS REPORT


      Jeshi la polisi nchini Tanzania limetoa tamko kwa wananchi wenye matatizo ya kupotelewa na mali zao. Jeshi hilo limeazimia kupunguza usumbufu na changamoto kwa raia kwa kuboresha uendeshaji wa huduma zao kwa wananchi.

     Jeshi la polisi limezindua mfumo mpya ambao utakua mwarobaini juu ya huduma ya loss report, ambapo jeshi hilo limewataka raia kutumia tovuti ya
 https://www.lormis.tpf.go.tz ambapo raia ataweza kujihudumia mwenyewe online kabla ya kwenda kituo cha polisi.


Thursday, 20 June 2019

UPDATE KUTOKA RITA TANZANIA



Taarifa muhimu kutoka RITA kwenda kwa waombaji wapya wa mkopo kutoka HESLB kwa mwaka 2019/2020.

Kupata maelezo zaidi Soma hapa👇


Thursday, 13 June 2019

Alexis the red_devil💪

This guy look to be angry with his last season's performance, now he is doing anything hardworking to return the status and honor... 2019/2020 EPL can't wait⚽

Tuesday, 11 June 2019

Elimu ya kijinsia

Sote ni wanadamu haijalishi umezaliwa mwanaume ama mwanamke, cha msingi tuheshimiane na kuacha kunyanyasana sababu ya jinsia. Hakuna jinsia ambayo ndiyo inapaswa kufanya kazi zote, tuasaidiane majukumu.