Sunday, 15 December 2019

AFYA: WALI NI HATARI ZAIDI KULIKO SODA KATIKA KUSABABISHA KISUKARI, FAHAMU JINSI YA KUJIKINGA



Katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kisukari mamlaka nchini Singapore zimeeleza kuwa mchele mweupe ni hatari zaidi kama kisababishi cha ugonjwa huo kuliko hata soda.
Watalaamu wa afya wameeleza kuwa kiribatumbo au vinywaji vyenye sukari ni visababishi vikubwa pia vya ugonjwa huo, hasa katika nchi za Magharibi. Lakini kwa upande wa nchi za Asia wali mweupe umekuwa ni tatizo kutokana na starch katika chakula hicho ambapo huijaza miili ya walaji na kiwango kikubwa cha sukari katika damu, na hivyo kuongeza hatari ya kupata Kisukari.
Katika tafiti nne zilizofanywa na Harvard School of Public Health na kuchapishwa katika jarida la afya la nchini Uingereza zilibaini kuwa, moja kila sahani moja ya wali inayoliwa kwa siku inaongeza uwezekano wa kupata kisukari kwa 11% kwa ujumla.
Pili, wakati raia wa Asia mfano wachina wakila wale kwa wastani wa mara nne kwa siku, wakazi wa Marekani na Australia hula chakula hicho kwa wastani wa mara tano kwa wiki.
Kutokana na hatari kubwa inayotokana na ulaji wa mchele mweupe, wataalamu wanashauri watu kupunguza kiwango cha ulaji wa chakula hicho. Mbali na hilo ambalo kwa baadhi ya watu linaweza kuwa gumu, wanashauriwa kuchanganya wali mweupe na wali wa ‘brown’ ili kupunguza kiwango cha sukari mwilini.
Ugonjwa wa Kisukari huchangia kupoteza uwezo wa mtu kuona, figo kushindwa kufanya kazi, pamoja na matatizo mengine ya kiafya.
Kuweza kujikinga na ugonjwa huo watu wanashauriwa kupunguza kiwango cha ulaji wa mchele mweupe, vinywaj vyenye sukari, pamoja na vyakula vya kisasa (junk foods).

No comments:

Post a Comment